Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

4 Septemba 2023

18:44:09
1391162

Ufaransa yaanza kutekeleza marufuku ya vazi la abaya, mashirika ya haki za binadamu yakosoa

Ufaransa leo imeanza kutekeleza marufuku la vazi la abaya linalovaliwa na wanawake wa Kiislamu, suala ambalo limekosolewa sana na Waislamu na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Marufuku ya vazi hilo imetajwa na makundi ya kutetea haki za binadamu kuwa ni mwendelezo wa sera ya kupiga vita Uislamu nchini Ufaransa ambayo imekuwa ikijinadi kuwa kirana wa uhuru na demokrasia. 

 Utekelezaji wa marufuku ya vazi la abaya kwa wanafunzi wa kike katika shule za umma inakuja baada ya Ufaransa kupiga marufuku alama za kidini katika shule na majengo ya serikali.

 Mapema leo Waziri wa Elimu wa Ufaransa, Gabriel Attal, amesema kuwa serikali inazifuatilia shule takribani 500 ambazo huenda zikakaidi amri hiyo wakati huu shule zinapofunguliwa. 

Awali, Rais Emmanuel Macron aliweka wazi kuwa wanafunzi watakaovaa mavazi aina ya abaya au buibui hawataruhusiwa kuingia madarasani. 

Mwaka 2004  nchi hiyo ilipiga marufuku wasichana kuvaa vazi la Hijab hasa katika shule zinazomilikiwa na serikali. Vazi la abaya ambalo linachukuliwa kuwa buibui la mtindo wa kisasa huvaliwa na baadhi ya wanawake wa Kiislamu kama stara.

Tangu Rais Emmanuel Macron aliposhika hatamu za uongozi nchini Ufaransa, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na hata kuvunjiwa heshima matukufu ya  Uislamu vimeongezeka mno katika nchi hiyo ya bara Ulaya.

342/