Main Title

source : Parstoday
Jumanne

5 Septemba 2023

13:15:24
1391408

Ufaransa yataka kuwepo makubaliano ya usalama baina ya Russia na Magharibi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema kuna udharura wa kutiwa saini makubaliano ya usalama baina ya nchi za Magharibi na Russia baada ya kumalizika vita nchini Ukraine.

Catherine Colonna amesema katika mahojiano na gazeti la Le Monde kwamba: "Vita vya Ukraine vitakapomalizika, itakuwa muhimu kwa viongozi wa nchi za Magharibi kuanisha muundo wa usalama unaoheshimu maslahi ya Russia."

Msimamo huu wa serikali ya Ufaransa unakwenda kinyume na ahadi ya serikali ya Paris ya kuiunga mkono Kiev kwa gharama yoyote ile.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa ameongeza kuwa: "Ukweli, historia na jiografia vyote vinaonyesha kwamba Russia iko katika bara la Ulaya. Hivyo tunahitaji kutafuta njia ya kuanzisha upya mfumo thabiti wa usalama unaozingatia maslahi na amani ya pande zote." 

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, amesisitiza tangu mwaka jana kwamba Ulaya inapaswa kujadili "jinsi ya kutoa dhamana kwa Russia watakati itakaporejea kwenye meza ya mazungumzo".

342/