Main Title

source : Parstoday
Jumatano

6 Septemba 2023

13:26:06
1391637

Mataifa zaidi ya 70 yashiriki mkutano wa Tanzania wa mifumo ya chakula Afrika

Maelfu ya washiriki kutoka mataifa zaidi ya 70 wanakutana katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam nchini Tanzania, kwa ajili ya mkutano mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wamewataka viongozi wa Kiafrika kuzipatia ufumbuzi changamoto za masoko baina ya nchi barani humo kwa kuweka sera wezeshi ambazo zitakuwa na manufaa kwa mkulima na mfanyabiashara wa mazao ya kilimo.

Wito pia umetolewa kwa nchi za Afrika kuhakikisha kuna upatikanaji wa chakula cha kutosha na kuendeleza biashara huru ili kuboresha usalama wa chakula na maendeleo ya uchumi barani Afrika.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango amezitaka nchi za Afrika kupitia mkutano huo kujadiliana kuhusu uwezekano wa kuondoa vikwazo vya biashara kupitia uondoshaji wa kodi zisizo za lazima.

Makamu wa Rais wa Tanzania amesema serikali za Afrika zinapaswa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwapa wakulima wadogo pembejeo za bei nafuu, maarifa, ujuzi na mitaji ili kuongeza tija katika mnyororo wa thamani wa uzalishaji chakula.

Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Nasoro Kitunda amesema kukosekana kwa mwelekeo wa pamoja wa sera na sheria katika masuala ya biashara ni changamoto kwa nchi za Afrika hali ambayo inaweza kuzuia maendeleo ya biashara baina ya mataifa hayo.

342/