Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

7 Septemba 2023

15:14:05
1391907

Wazayuni waendeleza unyama kwa kubomoa nyumba za Wapalestina

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameendelea na hatua zao za kinyama za kubomoa nyumba za wananchi wa Palestina huko Quds inayokaliwa kkwa mabavu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Al-Ahad, mabuldoza ya utawala wa Kizayuni yakkiungwa mkono na jeshi la utawala huo ghasibu, yamebomoa nyumba na vituo vya viwanda vya Wapalestina mashariki mwa Baytul-Muqaddas inayokaliwa kwa mabavu. Kitendo hicho kisicho cha kibinadamu, kinajiri siku mbili tu baada ya utawala ghasibu wa Kizayuni kubomoa au kutaifisha majengo 33 ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds inayokaliwa kwa mabavu kwa kisingizio cha kutokuwa na kibali cha ujenzi.

Utawala wa Israel unabomoa nyumba za raia wa Kipalestina katika eneo hilo lengo likiwa ni kuwaweka chini ya mashinikizo na kuwafukuza raia hao katika eneo hilo.

Utawala haramu wa Israel umekuwa ukibomoa nyumba za raia wa Palestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi mahali pake lengo kuu likiwa ni kubadili muundo wa kijiografia wa maeneo ya Palestina na kuyapa maeneo hayo sura ya Kiyahudi. 

Hii ni licha ya kwamba, azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linataja shughuli zote za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi iliyoghusubiwa ya Palestina kuwa ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo utawala haramu wa Israel unaendeleza ubabe wake kwa kuharibu nyumba za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni mahali pale na kutokana na uungaji mkono wa madola ya Magharibi hususan Marekani na udhaifu wa Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama.

342/