Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

8 Septemba 2023

10:46:41
1392084

Moscow: Marekani inatafakari kuwaua viongozi wa mapinduzi Niger

Shirika la Kijasusi la Russia nje ya nchi (SVR) limeonya kuwa, serikali ya Marekani inatafakari suala la kuwaua kigaidi viongozi walioongoza mapinduzi ya kijeshi nchini Niger.

Shirika hilo la kiintelijensia la Russia lilitoa indhari hiyo jana Alkhamisi na kueleza kuwa: Ikulu ya White House hairidhishwi na matukio katika koloni la zamani la Ufaransa (Niger), na haitaki kutegemea uingiliaji wa kijeshi wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

SVR ya Russia imebainisha kuwa, Washington inafadhilisha kutumia mtu au kundi litakalofanya mauaji hayo kwa niaba yake, badala ya nchi hiyo kushambuliwa kijeshi na ECOWAS. Jumuiya hiyo ya kikanda imekuwa ikisisitiza kuwa itaishambulia kijeshi Niger ili kurejesha madarakani kile inachoita utawala wa kikatiba, lakini mpaka sasa haijatekeleza kivitendo vitisho hivyo.

Mapinduzi ya Niger yalifanywa Julai 26, 2023 ambapo walinzi wa rais walimkamata Rais Mohammad Bazoum na kutangaza kuipindua serikali yake. Kufuatia mapinduzi hayo, Jenerali Abdul Rahman Tiani alitangaza kuchukua madaraka ya nchi.

Marekani inakula njama hizo katika hali ambayo, mapinduzi ya Niger yanaungwa mkono na raia wengi wa nchi hiyo ambapo, maelfu wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga vikali uwepo wa kijeshi wa vikosi vya Magharibi wakiwemo wanajeshi wa Ufaransa katika ardhi yao.

Waniger wengi wanamchukulia Bazoum kuwa kibaraka wa nchi za Magharibi hususan Ufaransa, hivyo wanaunga mkono kuondolewa kwake madarakani na kuzitaka nchi za Magharibi kutoingilia mambo ya ndani ya nchi yao.

Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) lina rekodi ya kufanya mauaji na majaribio ya mauaji ya kisiasa na kigaidi nje ya nchi. Shirika la Russia Today limesema kiongozi wa Kongo, Patrice Lumumba na Fidel Castro wa Cuba walilengwa mara kadhaa kuuawa na Marekani, kama ilivyofichuliwa na Kamati ya Kanisa miaka ya 1970.

342/