Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Septemba 2023

20:29:08
1392471

Moscow: Tumezima mashambulizi 21 na tumeua wanajeshi 630 wa Ukraine katika kipindi cha saa 24

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa, katika muda wa saa 24, jeshi la nchi hizo limezima mashambulio 21 ya Ukraine na kuua takriban wanajeshi 630 wa serikali kibaraka ya Kyiv.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema hayo kwenye taarifa yake ya jana Ijumaa na kutoa takwimu mpya za vifo, majeruhi na hasa ilizopata jeshi la Ukraine katika kipindi cha saa 24 za hadi wakati wa kutolewa taarifa hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema kwamba, kwa uchache operesheni 21 za jeshi la Ukraine zimezimwa na jeshi la Russia katika kipindi cha saa 24 kwenye maeneo ya Donetsk, Kupyansk, Zaporozhye, Krasnyi Lyman na Kherson.

Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kuwa, zaidi ya wanajeshi 630 wa Ukraine wameuawa na kiasi kikubwa cha vifaa vyao vya kivita vimeharibiwa wakati wajeshi wa serikali ya Kyiv walipojaribu kuwashambulia wanajeshi wa Russia.

Taarifa hiyo imesema kuwa ghala la kuhifadhia risasi za wanajeshi wa Ukraine katika mji wa Novodonetske wa Jamhuri ya Donetsk nalo pia limeteketezwa kwenye mashambulio ya anga ya Russia.

Hapo awali, mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliliambaia gazeti la "Kiev Post" kwamba katika kila ardhi ya ukumbwa wa mita 100 wanayoipata, huwa wanapoteza wanajeshi wanne hadi watano. Na huo ndio wastani wa hasara linazopata jeshi la Ukraine.

Alifafanua zaidi kuhusu kile alichokiita vita vya kulipiza kisasi vinavyoendelea hivi sasa kwamba, kila pale jeshi la Ukraine linaposimama na kutofanya harakati yoyote, huwa hakuna mwanajeshi anayeuawa isipokuwa majeruhi lakini mara tu linapoamua kusonga mbele hupata hasara kubwa.

342/