Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Septemba 2023

20:37:56
1392479

UNICEF: Ukatili dhidi ya watoto umekithiri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, vitendo vya ukatili dhidi ya watoto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimekithiri mno.

Shirika la UNICEF likitolea mfano watoto mapacha ambao hivi karibuni walikutwa wamefungwa mkanda wenye mabomu kiunoni ili yeyote atakayejaribu kuufungua uwezo kulipuka na kusababisha maafa limesisitiza kuwa, ukatili dhidi ya watoto umekithiri mno katika nchi hiyo.

Grant Leaity mwakilishi wa UNICEF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amebainisha kwamba, hivi karibuni alitembelea kituo kimoja katika jimbo la Kivu Kaskazini kinachohifadhi watoto walioachiliwa huru na vikundi vilivyojihami na kukuta watoto wawili mapacha wenye umri wa mwaka mmoja waliokuwa wametelekezwa kwenye Kijiji wakiwa na mkanda kiunoni wenye mabomu.

Amesema kuwa, kitendo hicho ni miongoni mwa ukatili dhidi ya watoto nchini DRC na kwamba ni taifa lenye matukio makubwa ya ukatili dhidi ya watoto yaliyothibitishwa na Umoja wa Mataifa.

Katika kipindi cha mwaka mmoja, ongezeko la ghasia mashariki mwa DRC limesababisha ukimbizi mkubwa zaidi Afrika, watoto zaidi ya milioni 2.8 wakibeba mzigo wa janga hilo.

Mwakilishi huyo wa UNICEF ameongeza kuwa, matumizi ya vilipuzi vya kutengeneza yanazidi kuongezeka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hivyo na hivyo UNICEF inatoa wito wa kuchukuliwa hatua ili kumaliza mzozo na familia zirejee nyumbani.

Takribani watoto milioni 1.2 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo uliokithiri kwenye eneo hilo.

342/