Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Septemba 2023

20:38:31
1392480

Wanaharakati wa Morocco waandamana kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Israel

Makumi ya wanaharakati wa Morocco wameandamana katika mji mkuu Rabat na kulaani kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walikusanyika mbele ya makao makuu ya Bunge la nchi hiyo na kutao nara za kulaani kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.

Aidha waandamanaji hao wakiwa na bendera ya Palestina wametangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina.

Waandamanaji hao wametangaza kuwa, wanapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel kwa namna yoyote ile.

Wananchi wa Morocco hadi sasa wameshaandamana na kumiminika mabarabarani mara kadha wa kadha sambamba na kuzichoma moto bendera za utawala haramu wa Kizayuni kuonyesha upinzani wao dhidi ya hatua ya serikali ya Rabat kuanzisha uhusiano wa kawaida na Tel Aviv na kutaka uhusiano huo ukomeshwe.

Hivi karibuni pia, baadhi ya wabunge wa Bunge la Morocco wamebainisha upinzani wao kwa hatua ya kuanzishwa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na wakatangaza kuwa kuanzisha uhusiano na utawala huo kutakuwa sawa na kupuuza mapambano ya watu wa Palestina na haki yao ya kuunda nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa ni Baitul Muqaddas.

Desemba 2020, Morocco na utawala haramu wa Israel zilifikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida kwa ushawishi wa Marekani. Na kama sehemu ya makubaliano hayo, Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump alikubali kutambua mamlaka ya Morocco juu ya Sahara Magharibi. Hata hivyo serikali ya rais wa sasa wa nchi hiyo Joe Biden imesema itauangalia upya uamuzi huo.

342/