Main Title

source : Parstoday
Jumapili

10 Septemba 2023

19:39:36
1392718

Watu 40 wauawa katika hujuma za anga Khartoum, Sudan

Watu wasiopungua 40 wameuawa katika mashambulizi ya anga kusini mwa Khartoum, mji mkuu wa Sudan.

Shirika la habari la Iran Press limeripoti habari hiyo leo Jumapili na kueleza kuwa, mbali na watu 40 kuuawa, makumi ya wengine wamejeruhiwa kwenye hujuma hizo za anga viungani mwa Khartoum.

Kamati ya Mapinduzi ambayo ilipata umarufu huko nyuma kwa kuandaa maandamano ya kuunga mkono demokrasia nchini Sudan imesema, "Mwendo wa saa 1:15 asubuhi, ndege ya kijeshi ilishambulia soko la Qouro na maeneo yanayopakana na soko hilo." 

Haya yanajiri siku chache baada ya Vikosi vya Radiamali ya Haraka vya Sudan RSF kutangaza kuwa wanachama wake wametungua ndege ya kivita ya jeshi la nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Mapigano ya silaha ya kuwania madaraka nchini Sudan yamekuwa yakiendelea tangu Aprili 15 kati ya vikosi vya jeshi na vya RSF. Maelfu ya watu wameuawa na mamia ya maelfu ya wengine kukimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo.

Mapigano hayo ambayo yameenea katika maeneo tofauti ya Sudan yakijikita zaidi katika mji mkuu Khartoum, yangali yanaendelea licha ya Jenerali Abdul Fattah al-Burhan, mkuu wa baraza la uongozi la Sudan kutoa taarifa ya kuvivunja Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF.

Hata hivyo Baraza la Ushauri la Vikosi vya Msaada wa Haraka limesema uamuzi huo wa al-Burhan unaenda kinyume na katiba ya Sudan, na kwa msingi huo hautatekelezwa.

342/