Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

11 Septemba 2023

14:15:32
1392986

Marekani yaendelea kuiba mafuta ya Syria mchana kweupe

Wanajeshi vamizi wa Marekani wanaendelea kuiba mafuta ya Syria ambapo katika tukio la karibuni kabisa, dola hilo "jizi na poraji" la Marekani limeonekana likisafirisha malori 95 ya mafuta ya Syria na kuingia nayo Iraq katika wizi wa mchana kweupe mbele ya kimya cha kuchukiza cha jamii ya kimataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, wanajeshi wa wanaoyakalia kwa mabavu maeneo mbalimbali ya Syria, jana (Jumapili), walisafirisha makumi ya malori ya waliyoyaiba katika visima vya mafuta vya Syria na kuyaingia nchini Iraq kwa ajili ya kuhamishia maeneo mengine.

Nalo Shirika la Habari la Syria (SANA) limenukuu duru za ndani ya nchi hiyo zikiripoti kwamba, jana asubuhi jeshi la Marekani lilituma msafara mpya wa mafuta ya Syria kuelekea nchini Iraq kwa kupitia kivuko haramu cha "Al-Mahmoudiyya." Mafuta hayo ni yale waliyoyaiba Wamarekani katika visima vya mafuta vya mashriki mwa Syria. Wamesafirisha mafuta hayo chini ya ulinzi mkali wa kijeshi.

Duru hizo za ndani ya Syria zimesema kuwa, awali Marekani ilipeleka msafara wa malori 40 ya mafuta ya Syria hadi Iraq na saa chache baadaye walituma msafara wa malori 55 ya mafuta waliyoyaiba nchini Syria kupitia kivuko hiyo hiyo cha Al Mahmoudiyya.

Wanajeshi wa Marekani wako nchini Syria kivamizi. Hawana kibali chochote cha kuweko nchini humo, si kutoka kwa serikali halali ya Syria na wala si kwa idhidi ya Umoja wa Mataifa. Dola jizi na vamizi la Marekani linaendelea kuiba utajiri wa mafuta wa wananchi wa Syria katika hali ambayo wananchi hao Waislamu wanateseka hivi sasa kwa uhaba mkubwa wa nishati na kwa vita vya miaka mingi ambavyo vilianzishwa na madola hayo hayo ya kibeberu yakiongozwa na Marekani, dhidi ya taifa hilo la Kiarabu.

342/