Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

11 Septemba 2023

14:25:51
1392993

Dhirisho la Umoja katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussain AS nchini Kenya

Maombolezi ya Arubaini ya Imam Husseini (AS) huko Nairobi, Kenya, yamefanyika kwa kuhudhuriwa na Waislamu wa madhehebu za shia na Suni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Iranpress, maombelezo ya Arubaini ya kuuwawa shahidi Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (AS) na wafuasi wake yamefanyika kwa kuhudhuriwa na Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni wapenzi wa Ahlul Bayt (AS) huko Nairobi na maeneo mengine ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Waislamu wa madhehebu ya suni wapenzi wa Ahlul Bayt pia walishiriki katika maombolezi hayo.

Kushiriki Waislamu wa madhehebu ya Suni katika maombolezo ya Arubaini ya imam hussein (AS) kando ya Waislamu wenzao wa madhehebu ya Shia kunaonyesha umuhimu wa kihistoria wa  tukio la Karbala ambalo linamgusa kila binadamu mpenda uhuru, na kudhihirisha kujitolea kwa Imam Husseini AS.

Wazungumzaji katika shughuli hiyo pia wameelezea kuwa maombolezo ya kuuliwa shahidi mjukuu huyo wa Mtume Muhammad (SAW) ni uwanja wa kuimarisha umoja kati ya waislamu. 

Inafaa kukumbusha kuwa tarehe 6 Septemba 2023 iliyosadifiana na tarehe 20 Safar mwaka 1445 ilikuwa ndio Arubaini ya Shahada ya Imam Hussein (AS) na wafuasi wake watiifu katika jangwa la Karbala hapo mwaka 61 Hijria.

342/