Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Septemba 2023

18:06:22
1393495

Umasikini waendelea kuongezeka nchini Marekani

Mfumuko mkubwa wa bei nchini Amerika umesababisha kupungua kwa wastani wa mapato halisi ya familia na kuongezeka kwa umaskini katika nchi hiyo.

Kanali ya Televisheni ya al-Mayadeen imeinukuu Idara husika nchiini Marekani ikitangaza kuwa, mfumuko wa bei na ughali wa maisha ulipunguza mapato halisi nchini Merika kwa asilimia 2.3 mnamo 2022 licha ya kuongezwa mishahara. Ofisi ya Sensa ya Marekani imetangaza kuwa, umaskini nchini humo uliongezeka hasa kutokana na kusitishwa kwa misaada ya serikali wakati wa janga la virusi vya Corona.

Liana Fox, afisa wa Ofisi ya Sensa ya Marekani, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba mfumuko wa bei wa juu nchini Marekani ulisababisha kupungua kwa wastani wa mapato halisi ya familia, ambayo yalifikia dola 47,960.Kiwango rasmi cha umaskini nchini Marekani kimesalia kuwa 11.5% ikilinganishwa na mwaka jana; Hiyo ina maana kwamba watu milioni 37.9 wanaishi chini ya kipato cha dola 14,880 kwa mwaka, au dola 29,950 kwa familia ya watu wanne. Kulingana na ripoti hii, kiwango cha umaskini kiliongezeka kwa mara ya kwanza tangu 2010 na kuongezeka kutoka 7.8% hadi 12.4% kati ya 2021 na 2022. Baa la njaa na kuongezeka umasikini limegeuka na kuwa tatizo kubwa linaloikumba Marekani kwa sasa. Hali hii imeifanya Marekani ikumbwe na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, maelfu ya Wamarekani kukosa ajira na kuongezeka umasikini na tofauti za kimatabaka katika nchi hiyo.

342/