Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

14 Septemba 2023

11:45:39
1393666

Kashfa ya ngono katika hospitali za Uingereza, ubakaji waripotiwa katika vyumba vya upasuaji

Utafiti uliofanywa na British Journal of Surgery (BJS) unaonyesha kuwa, karibu theluthi moja ya madaktari wa upasuaji na wahudumu wa chumba cha upasuaji katika hospitali za umma za Uingereza wamekuwa waathiriwa wa ubakaji au aina fulani ya unyanyasaji wa kijinsia.

Utafiti wa British Journal of Surgery unaonyesha kuwa, 63% ya wanawake walikuwa wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia waliofanyiwa na wenzao, 30% ya wanawake wamebakwa, 11% wameripoti kulazimishwa kupapaswa mwili kwa ajili ya kupata fursa na nafasi za kazi, na 90% ya wanawake na 81% ya wanaume wameshuhudia aina fulani ya unyanyasaji wa kijinsia.

Baada ya kuchapishwa ripoti hii, baadhi ya madaktari wa upasuaji wa kike wa Uingereza wamesema kwamba, kesi zilizoripotiwa zimefichua sehemu ndogo sana ya unyanyasaji wa kingono unaofanyika katika vyumba vya upasuaji vya hospitali za umma nchini Uingereza.

Uchunguzi wa maoni uliohusisha madaktari wa upasuaji wa kike na wafanyakazi wapatao 1,700 katika vyumba vya upasuaji vya hospitali za umma za Uingereza unaonyesha kwamba, ukatili na unyanyasaji wa kingono wa madaktari wa upasuaji wa kike na wafanyakazi hauishii katika hospitali za nchi hiyo, bali wanawake wanakabiliwa na tatizo hilo la ukatili wa wenzao wanaume katika maeneo mengine.Waziri wa Sayansi, Ubunifu na Teknolojia wa Uingereza, Michelle Donelan, amesema baada ya kufichuliwa kwa kashfa hii kwamba: "Hili ni suala la kusikitisha sana, na ninataka wafanyakazi wote katika idara za upasuaji za hospitali kuripoti unyanyasaji wa kijinsia." Kwa upande wake, Rachael Venables, mtaalamu wa vyombo vya habari, ameashiria ripoti hiyo na kusema: Idadi kubwa ya wafanyakazi wa idara ya upasuaji ya Shirika la Kitaifa la Afya nchini Uingereza ama walikuwa wahanga wa unyanyasaji wa kingono au walishuhudia unyanyasaji wa aina hiyo, ambao umeathiri vibaya afya yao wa kimwili na kiakili.