Main Title

source : Parstoday
Jumapili

17 Septemba 2023

19:27:42
1394175

Macron adai waliofanya mapinduzi Niger "wanamshikilia" balozi wa Ufaransa

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alidai jana Ijumaa kwamba balozi wa nchi yake nchini Niger, Sylvain Itte, "anazuiliwa" na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika, akiashiria kwamba chakula anachokula ni "mgao wa chakula cha kijeshi."

Macron ameongeza kwamba, nchi yake ina balozi na wafanyakazi wa kidiplomasia "wanaozuiliwa" katika ubalozi wa Ufaransa huko Niamey, na  kwamba jeshi lla Niger inamezuilia chakula wanadiplomasia hao.

Itakumbukwa kuwa mwezi uliopita wa Agosti watawala wa kijeshi wa Niger walimwamuru mabalozi wa Ufaransa kuondoka nchini humo ndani ya masaa 48, huku uhusiano kati ya Niamey na mkoloni huyo wa zamani ukiendelea kuharibika.

Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Ufaransa kuendeleza fikra zake za kikoloni na kutoheshimu amri za serikali mpya ya Niger iliyoingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum ambaye wananchi wa Niger wanasema alikuwa kibaraka mkubwa wa Ufaransa.

Ufaransa ilipinga uamuzi huo mara moja, ikisema kwamba haitambui mamlaka ya watawala hao wa kijeshi. 

Polisi nchini Niger wanaendelea kuzingira majengo ya ubalozi wa Ufaransa mjini Niamey, huku Baraza la Kijeshi linalotawala nchi hiyo likichukua uamuzi wa kupiga marufuku shughuli za mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali.

Maelfu ya wananchi wa Niger wamekuwa wakifanya maandamano karibu na kambi ya jeshi la Ufaransa katika mji mkuu Niamey kwa lengo la kutangaza uungaji mkono wao kwa serikali ya kijeshi na kutaka wanajeshi wa Ufaransa waondoke mara moja katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.Tarehe 26 Julai 2023, walinzi wa rais wa Niger walifanya mapinduzi dhidi ya rais wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum; na mkuu wa walinzi hao, Jenerali Abdourahamane Tchiani, alijitangaza kuwa kiongozi mpya wa nchi na mkuu wa baraza la mpito.

342/