Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

18 Septemba 2023

16:27:35
1394401

Maandamano makubwa ya wanaharakati wa mazingira katika kukaribia mkutano wa UNGA

Malefu ya wanaharakati wa mazingira wameandamana kabla ya kuanza Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) mjini New York, Marekani kwa lengo la kuhitimisha matumizi ya fueli za kisukuku.

Katika mjumuiko huo wa wanaharakati wa kutetea mazingira ambao ni sehemu ya maandamano makubwa ya wiki nzima ambayo yanatazamiwa kufanyika pia katika nchi nyingi, baadhi ya wanaharakati wa mazingira walikuwa na mabango yenye maandishi yanayosema: "Sitisha matumizi ya fueli za kisukuku", "fueli za kisukuku zinaua" na "tangazeni dharura ya mabadiliko ya tabia nchi." 

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, zaidi ya maandamano 500 yamepangwa kufanyika katika nchi 54 ikiwemo Marekani, Ujerumani, Uingereza, Korea Kusini na India; ambapo lengo la maandamano hayo ni kuchukukuliwa hatua za haraka ili kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la joto duniani.   

Maandamano hayo yanafanyika ambapo inatazamiwa kuwa miezi miwili ijayo Umoja wa Mataifa utaitisha Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi kwa jina la Mkutano wa COP28.  

Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulitahadharisha kuwa dunia inaelekea kukumbwa na joto kali na kwamba kuna ulazima wa kuchukuliwa hatua kubwa katika nyanja zote ikiwemo kupunguza matumizi ya makaa ya mawe kama mbadala wa fueli.  

Wasomi wengi wanaamini kuwa gesi ya nyumba ya kijani zinazotokana na fueli za kisukuku zinasababisha ongezeko la joto na maafa ya kimaumbile kama mafuriko, ukame na moto wa misituni.  

342/