Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

18 Septemba 2023

16:27:57
1394402

Patrushev: Marekani inazitumia vibaya nchi wanachama wa Nato

Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia ametangaza kuwa upanuzi usio na kikomo wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) umetoa mwanya kwa Marekani kuzifanya nchi nyingi kuwa vibaraka wake.

Nikolai Petrushev ameeleza kuwa, Magharibi mara nyingi hukimbilia kutumia nguvu za kijeshi, vitisho na mabavu, vikosi maalumu na mapinduzi ya rangi ili kudhibiti ulimwengu. 

 Afisa huyo wa Russia piia amekosoa kambi ya kijeshi inayoongozwa na Marekani kwa kile alichokiita "unafiki," na kusema kuwa wakati NATO inadai kuwa inaunga mkono amani, inaendesha vita dhidi ya nchi zinazopinga sera za Washington duniani huku ikitishia kuanzisha vita na kuchukua hatua za kijeshi.   

Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia ameongeza kuwa, nchi wanachama wa NATO katika miongo saba iliyopita zimeshiriki na kupigana vita zaidi ya mara 200 katika maeneo mbalimbali duniani. Amesema nchi za Magharibi zinaiona Russia kuwa ni tishio la kudumu kwa sababu nchi hizo zinakumbuka kuwa Umoja wa Kisovieti ulikuwa na jukumu muhimu katika kuharibu mfumo wa kikoloni. 

342/