Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

18 Septemba 2023

16:31:38
1394409

Wazayuni wakasirishwa na uamuzi wa UNESCO

Uamuzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wa kuingiza eneo la kihistoria la Palestina katika Orodha ya Turathi za Dunia umeukasirisha utawala wa Kizayuni.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa uamuzi wa kuuweka muinuko wa  Al-Sultan (Tal al-Sultan) huko Jericho (Ariha) katika urithi wa dunia ulitolewa katika mkutano wa 45 wa Kamati ya Turathi za Dunia, uliofanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia, ambapo ujumbe wa utawala wa Kizayuni ulishiriki pia.  

Ernesto Otten, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la UNESCO, alisema katika mkutano huo kwamba: Hapa ni mahali panapopendekezwa kujumuishwa katika urithi wa dunia, Tal al-Sultan ya kale, ambayo ilianzia nyakati za kabla ya historia na iko nje ya eneo la kale la Jericho (Ariha).  

Wakati huo huo, Otten amebainisha kuwa: Hakuna athari zozote zilizosalia za Wayahudi na Wakristo katika eneo hili, bali athari zilizopo katika eneo hili ni zile za kipindi cha historia kati ya miaka 10,000  hadi mia saba kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (as). 

Eneo la Tal al-Sultan liko kilomita 10 kaskazini mwa Bahari ya Chumvi na kilomita 2 kaskazini katikati mwa mji wa Ariha.

342/