Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

22 Septemba 2023

15:47:49
1395005

Marekani yatangaza kusitisha ushirikiano wake wa kijeshi na Rwanda; DRC yapongeza

Marekani imetangaza kusitisha ushirikiano wake wa kijeshi na Rwanda kwa tuhuma kwamba Kigali inawatumia watoto kama wanajeshi na kuunga mkono waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Rwanda imeongezwa kwenye orodha ya nchi 19 ambazo Marekani imesitisha ushirikiano wake wa kijeshi iliokuwa nao na nchi hizo, baada ya kupata ushahidi kuwa Kigali huwatumia watoto katika vikosi vyake au makundi yanayobeba silaha ambayo serikali hiyo inayaunga mkono.

Afisa huyo wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amebainisha kuwa, Rwanda imeongezwa kwenye orodha hiyo kutokana na jeshi lake la RDF kuunga mkono kundi la waasi wa M23 mashariki ya DRC ambalo linatuhumiwa kufanya mauaji ya raia na pia limekuwa likisajili watoto kuwa wapiganaji wake.

Mwaka 2013 Washington ilichukua hatua hiyohiyo dhidi ya Rwanda kwa tuhuma sawa na hizo.

Hata hivyo Rwanda imeendelea kukanusha madai ya kuliunga mkono kundi la waasi wa M23, wakati ripoti ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa zaidi ya watoto 17,500 wameondolewa kwenye makundi ya waasi tangu mwaka 2017.

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amepongeza hatua hiyo ya Marekani ya kusitisha ushirikiano wake wa kijeshi na Rwanda.../

342/