Kiongozi
huyo wa mpito wa Guinea ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini
New York kwamba bara hilo lilikuwa likiteseka kutokana na "mfano wa
utawala uliotwikwa juu yetu" na ambao "hauendani na hali halisi ya
mambo".
"Wakati umewadia muache kutusomea na kutufanya kama watoto," aliongeza.
Kanali Doumbouya alichukua mamlaka katika mapinduzi mwaka wa 2021, na kumuondoa madarakani Rais Alpha Condé.
Alitetea hatua hiyo katika kikao cha Umoja wa Mataifa akisema ni "kuokoa nchi yetu kutokana na machafuko kamili".
Wakati huo, habari za mapinduzi zilipokelewa kwa furaha na umati wa watu katika mji mkuu, Conakry, kwani wengi walikuwa wamefarijika kwamba Rais Condé alikuwa ameondolewa.
Lakini nchi hiyo iliondolewa katika jumuiya ya kikanda, Ecowas, baada ya jeshi kuchukua hatamu, huku viongozi wa kikanda wakitaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.
Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi mwaka juzi baadaye aliachiliwa huru kutoka kifungo cha nyumbani baada ya ushikiliwa kwa takkribani wikii moja.
Guinea ni miongoni mwa nchi kadhaa za magharibi na kati mwa Afrika ambazo zimeshuhudia mapinduzi katika miaka ya hivi karibuni zikiwemo Mali, Burkina Faso, Niger na Gabon. Mapinduzi hayo yalilaaniwa vikali na Ecowas, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.
342/