Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

23 Septemba 2023

18:26:59
1395372

Ripoti: Vifaru vya kivita vya UK vina mada za sumu

Gazeti la The Times limefichua kuwa, maelfu ya vifaru vya kivita vya Uingereza vina mada za sumu ambazo ni hatari kwa afya ya mwanadamu.

Gazeti hilo limemnukuu James Cartlidge, Waziri wa Zabuni za Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ambaye ameeleza kuwa, mada hatarishi ya asbestos ipo katika vifaru na magari ya deraya 2,699 ya Jeshi la UK.

Habari zaidi zinasema kuwa, baadhi ya vifaru hivyo vyenye mada za sumu tayari vimekabidhiwa Ukraine. Mada za sumu za asbestos (ACMs) zinaripotiwa kuwa hatari kwa afya ya mwanadamu hasa kwa mapafu.

Waziri Kivuli wa Ulinzi wa Uingereza, John Healey amesema kiwango cha mada za asbestos zilizoko katika silaha za zana za kijeshi za Uingereza ni cha kutisha na kutia wasiwasi. 

Serikali ya Kyiv imeendelea kutoa wito kwa washirika wake wa Magharibi kuipatia vifaa vingi vya kisasa vya kijeshi ili kusaidia vikosi vya Ukraine kutwaa tena maeneo makubwa yanayodhibitiwa na vikosi vya jeshi la Russia.

Haya yanajiri wakati huu ambapo utumiaji wa mabomu ya vishada katika vita vya Ukraini na matokeo yake hatari yamewakasirisha watetezi wengi wa haki za binadamu na hata taasisi za kimataifa.Hivi karibuni, Izumi Nakamitsu, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alionya kuhusu hatua ya nchi za Magharibi ya kuipa Ukraine silaha hizo na kutaka matumizi yake yasimamishwe mara moja. Alisema silaha hizo ni hatari kwa maisha ya mwanadamu na zinapaswa kufutwa kabisa katika historia.

Hata hivyo Msemaji wa Usalama wa Taifa ya Ikulu ya White House ya Marekani, John Kirby hivi karibuni alipongeza na kusifu uamuzi wa Washington wa kutuma mabomu hayo yaliyopigwa marufuku kimataifa ya vishada nchini Ukraine.



342/