Main Title

source : Parstoday
Jumanne

26 Septemba 2023

19:10:22
1396022

WHO yataka marufuku ya sigara za aina zote shuleni

Leo, Ili kusaidia kulinda afya ya Watoto, Shirika la Umoja wa Matafa la Afya Ulimwenguni limetoa machapisho mawili mapya, “Uhuru dhidi ya tumbaku na nikotini: mwongozo kwa shule,” na “zana za shule zisizo na nikotini na tumbaku.”

Sekta ya tumbaku inawalenga vijana kwa tumbaku na bidhaa za nikotini na kusababisha matumizi ya sigara ya kielektroniki kuongezeka kwa wavutaji 9 kati ya 10 wanaoanza kabla ya umri wa miaka 18.

“Bidhaa za tumbaku pia zimefanywa kuwa nafuu kwa vijana kupitia uuzaji wa sigara za kawaida na za umeme na kibaya zaidi haziambatani na maonyo ya kiafya.” Inasema WHO. 

Shirika hili la afya ulimwenguni linatoa mfano wa hivi karibuni ambapo Mamlaka za usimamizi nchini Marekani mwezi uliopita zimeonya makampuni kuacha kuuza sigara za kielektroniki ambazo zimeundwa kwa mfanano wa vifaa vingine vya shule na hivyo kuwavutia vijana. Pia ziko sigara nyingine zimeundwa kwa muonekano wa vikaragosi au katuni zinazopendwa na watoto au vijana.

Dkt Ruediger Krech, Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Afya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni ameonya kwa kusema: "Iwe kukaa darasani, kucheza michezo nje au kusubiri kwenye kituo cha basi la shule, lazima tuwalinde vijana dhidi ya moshi mbaya wa sigara na utokaji wa sumu ya sigara ya kielektroniki pamoja na matangazo yanayotangaza bidhaa hizi."

Mwongozo mpya na zana ni miongozo ya hatua kwa hatua kwa shule kuunda maeneo yasiyo na nikotini na tumbaku, lakini inahitaji mbinu ya "shule nzima" - ambayo inajumuisha walimu, wafanyakazi, wanafunzi, wazazi na kadhalika. Mwongozo na zana ni pamoja na mada kuhusu jinsi ya kusaidia wanafunzi kuacha kuvuta sigara, kampeni za elimu, utekelezaji wa sera na jinsi ya kuzitekeleza.

Ili kulinda afya ya watu, WHO inahimiza nchi zote kufanya maeneo yote ya umma ya ndani yasiwe na moshi kabisa kulingana na Kifungu cha 8 cha Mkataba wa Mfumo wa WHO wa Kudhibiti Tumbaku.