Main Title

source : Parstoday
Jumanne

26 Septemba 2023

19:10:45
1396023

Ujerumani yakiri kuipatia Ukraine zana kongwe za kijeshi

Waziri wa Mambo ya Nje ya Ujerumani amesema kuwa nchi yake imetuma Ukraine zana na silaha za zamani ambazo hazifanyi kazi kama msaada wa kijeshi kwa nchi hiyo.

Imepita miezi 17 sasa tangu kuanza vita kati ya Russiai na Ukraine huku watu elfu kumi wakiwa wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi, hata hivyo Kiev na waitifaki wake wa Magharibi zinaendelea kupinga mapendekezo yaliyowasilishwa na nchi kadhaa kwa ajili ya  kusitisha vita na kurejesha amani huko Ukraine.  

Vita vya Ukraine vinatajwa kuwa ni fursa ya kupakua na kutumiwa silaha za zamani za nchi nyingi za Ulaya za Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO na pia kutumiwa silaha zinazoundwa na makampuni ya Marekani. 

Annalena Baerbock Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amekiri katika mahojiano aliyofanyiwa kwamba Berlin imeipatia mara kadhaa serikali ya Kiev silaha na zana za kijeshi za zamani na kongwe na kwamba walijua tangu awali kuwa baadhi ya silaha hizo haziwezi kutumika. 

Mwezi Aprili mwaka jana Russia ilituma barua ya kidiplomasia kwa nchi zote wanachama wa Nato kuhusiana na hatua yao ya kutuma silaha huko Ukraine. Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov alisema shehena yoyote ya silaha inayotumwa Ukraine itakuwa mlengwa wa mashambulio ya Russia. 

342/