Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

28 Septemba 2023

16:55:21
1396458

Russia yalaani sera za kinafiki za Magharibi kuhusu migogoro ya Syria na Ukraine

Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa sababu ya nchi za Magharibi kupuuza mahitaji ya kibinadamu ya Syria ni kuelekeza mazingatio yao kwa nchi ya Ukraine.

Dmitry Polyanskiy amesema leo Alkhamisi katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba nchi za Magharibi zinapuuza mahitaji ya kimsingi ya watu wa Syria ili ziendelee kutuma misaada ya silaha kwa serikali ya Ukraine.

Polyanskiy amesisitiza kuwa: "Ni dhahiri kwamba Syria na nchi nyingine kadhaa zinazohitaji misaada ya kibinadamu zinakabiliwa na ubaguzi mkali na nchi za Magharibi, kwa sababu Wamagharibi wanajishughulisha tu na suala la kutuma silaha nchini Ukraine."

Mwanadiplomasia huyo wa Russia amedokeza kuwa, mpango wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Syria mwaka huu umetengewa chini ya asilimia 30 ya bajeti, na hii inaonyesha hali mbaya ya mtazamo wa Wamagharibi.

Hapo awali, chanzo cha habari kililiambia shirika la habari la Russia, Ryanovsky, kwamba Marekani inazitishia nchi za Kiarabu kwamba hazipaswi kusaidia mchakato wa kuijenga upya Syria au kutoa msaada wa kifedha kwa serikali ya nchi hiyo.

342/