Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

29 Septemba 2023

22:19:09
1396694

Wataalamu: Uwezekano wa kuuawa na polisi Wamarekani weusi ni mara 3 zaidi ya Wamarekani weupe

Mfumo wa kibaguzi dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika umepenyezwa hadi kwenye utendaji wa jeshi la polisi na mfumo wa mahakama nchini Marekani.

Ripoti mpya ya wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imeakisi ubaguzi mkubwa wanaofanyiwa Wamarekani weusi na kueleza kkwamba, lazima marekebisho ya haraka yafanywe ili kuondokana na raia hao wa Marekani.

Katika ripoti hiyo Baraza la Haki za Binadamu la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wao kutokana na takwimu na mazingira ambayo watu wanauawa na polisi nchini Marekani.Ripoti hiyo inaeleza kuwa Wamarekani Weusi wana uwezekano wa kufungwa jela mara 4.5 zaidi ya wazungu. Kulingana na ripoti maalum ya Idara ya Haki, watu weusi wana uwezekano mara tatu zaidi wa kukabiliwa na tishio la kulazimishwa na wana uwezekano mara 11 zaidi wa kukabiliwa na vitendo vya utovu wa nidhamu kutoka kwa polisi kama vile matusi, chuki au tabia mbaya ya kingono kuliko watu weupe. Takwimu za hivi karibuni nchini Marekani zinaonyesha kuwa, watu weusi wanaunda asilimia 90 ya wafanyakazi walioachishwa kazi mwaka huu kutokana na kuongezeka kwa hofu ya mdororo wa kiuchumi na sera ya makampuni mengi ya kupunguza wafanyakazi. Vilevile ubaguzi wa rangi umetajwa kuwa moja ya sababu muhimu za vifo vya akina mama wajawazito weusi huko Marekani, kwa kadiri kwamba Umoja wa Mataifa umetangaza katika muktadha huu kuwa, kiwango kikubwa cha vifo vya wajawazito kati ya wanawake weusi huko Amerika Kaskazini kinatokana na ubaguzi wa rangi kwa njia ya unyanyasaji wa kimaneno na kimwili wa watoa huduma za afya, pamoja na kunyimwa huduma bora na dawa za kutuliza maumivu.

342/