Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

2 Oktoba 2023

19:13:10
1397470

Madaktari na wataalamu wa afya wagoma kufanya kazi Uingereza

Madaktari na wataalamu wanaofanya kazi katika sekta ya afya ya umma nchini Uingereza wamegoma wakipinga gharama za maisha, kutolipwa mishahara na mazingira duni ya kazi.

Mgomo wa siku tatu wa madaktari na wataalamu wanaofanya kazi katika mfumo wa huduma za afya ya umma nchini Uingereza umeanza leo asubuhi sambamba na kufanyika mkutano wa kila mwaka wa chama tawala cha Kihafidhina cha nchi hiyo. Madaktari na wataalamu wa afya waliogoma huko Uingereza wamesema kuwa ni karibu muongo mmoja sasa ambapo mishahara yao haijaongezwa; na kwa kuzingatia kuwa mfumuko wa bei umefika kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, mishaha yao inapaswa kuongezwa angalau kulingana na kasi ya mfumuko wa bei. Hata hivyo Wizara ya Afya na Tiba ya Uingereza imetangaza kuwa mishahara ya madaktari itaongezwa kwa asilimia 9 na wataalamu wa tiba kwa asilimia 6. Viwango hivi vimetajwa kuwa vidogo sasa ikilinganishwa na gharama za maisha hasa kupanda kwa bei za vyakula na nishati. Hadi sasa zimepita siku 100 tangu kufanyika mkutano wa mwisho wa wawakilishi wa serikali na Shirika la Mfumo wa Matibabu la Uingereza kuhusu ufuatiliaji wa maombi ya madaktari na wataalamu wa tiba. Wakati huo huo mazungumzo kati ya pande hizo mbili ili kutatua suluhiisho la hali hiyo hadi sasa hayajazaa matunda. Kesho Jumanne wafanyakazi wa sekta ya Radioloji wa Uingereza wamepanga kufanya mgomo kulalamikia ongezeko la gharama za maisha, hali mbaya ya utendaji kazi na mishahara midogo. 

342/