Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

2 Oktoba 2023

19:13:41
1397471

Erdogan: Uturuki haitarajii chochote kutoka Umoja wa Ulaya

Rais Recep Tayyeb Erdogan wa Uturuki amesema taifa hilo halitazamii kupata kitu chochote kutoka Brussels, baada ya kusubiri kwa miongo kadhaa kupewa uanachama wa Umoja wa Ulaya.

Erdogan alisema hayo jana Jumapili katika hotuba yake kwa taifa kupitia Bunge la nchi hiyo na kueleza kuwa, "Tumetimiza ahadi zote tulizoiahidi EU, lakini wao hawajatekeleza ahada zao."

Mchakato wa kujiunga Uturuki na Umoja wa Ulaya na hasa katika miongo kadhaa ya karibuni umekabiliwa na vizuizi na ucheleweshaji mkubwa. Rais wa Uturuki ameeleza bayana kuwa, "Hakuna anayetarajia chochote kutoka kwa Umoja wa Ulaya, ambao wametufanya tusubiri katika mlango wao kwa miaka 60."

Kwa mujibu wa ripoti ya Bunge la Ulaya, taasisi hiyo inaamini kuhusu uhusiano wake na serikali ya Ankara kwamba, mchakato wa kujiunga Uturuki na Umoja wa Ulaya 'umefungwa na kusimamishwa' na kwamba mchakato mwingine mbadala unapasa kutafutwa.  Katika muongo mmoja uliopita, hatua ya serikali ya Ankara chini ya uongozi wa Recep Tayyep Erdogan ya kutekeleza sera huru mkabala wa serikali za Magharibi imezitia wasiwasi na kutoziridhisha Marekani na Umoja wa Ulaya. Rais Erdogan amewahutubu viongozi Umoja wa Ulaya kwa kuwaambia: Waliopo Brussels wanaweza kurekebisha makosa yao iwapo wataacha kuamiliana na Uturuki kwa mienendo isiyo ya kiadilifu, hasa juu ya suala la utoaji viza kwa raia wa Uturuki. Wasipobadilika, watapoteza haki ya kutarajia chochote kutoka kwetu. 

342/