Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

2 Oktoba 2023

19:14:04
1397472

Medvedev: Hatua za Uingereza zinaharakisha vita vya tatu vya dunia

Rais wa zamani wa Russia, Dmitry Medvedev, ameonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita vya tatu vya dunia, akitoa maoni yake juu ya matamshi yaliyotolewea na Uingereza kuhusu kutuma wakufunzi wa kijeshi katika ardhi ya Ukraine.

Dmitry Medvedev amesema kwamba wanajeshi wa Uingereza watakaotumwa Ukraine watakuwa shabaha halali kwa vikosi vya jeshi la Russia.

Medvedev, ambaye sasa anashikilia wadhifa wa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Russia, amesema kwamba vikosi vya jeshi la Russia vitawashughulikia wanajeshi wa Uingereza wanaotoa mafunzo kwa vikosi vya Ukraine "bila huruma."

Medvedev ameeleza - ​​kupitia mtandao wa Telegram - kwamba hatua kama hizo za Magharibi zinaharakisha kuibuka kwa vita vya tatu vya dunia.

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Russia amesema kwamba iwapo Kiev itapewa makombora ya Taurus kushambulia Russia, mashambulio dhidi ya viwanda vinavyozalishaji makombora hayo vya Ujerumani "yataafiikiana na sheria za kimataifa."

Itakumbukwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Grant Shapps, alisema Jumamosi iliyopita kwamba, amefanya mazungumzo na makamanda wa jeshi kuhusu suala la kutuma vikosi vya jeshi la Uingereza ndani ya ardhi ya Ukraine katika programu ya mafunzo.

342/