Main Title

source : Parstoday
Jumatano

4 Oktoba 2023

17:36:37
1397919

Baraza la Wawakilishi la Marekani lamuuzulu Spika wake kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani jana Jumanne walipiga kura kwa wingi na kumuuzulu Spika Kevin McCarthy, hatua ambayo ni ya kwanza ya aina yake katika historia ya nchi hiyo.

Baraza la Wawakilishi limemuuzulu aliyekuwa spika wake, McCarthy, kwa kura 216 dhidi ya 210 za kupinga.

Kevin McCarthy anakuwa Spika wa kwanza wa Baraza la Wawakilishi katika historia ya Marekani kutimuliwa kwenye nafasi hiyo na wenzake kwa mpango ulioandaliwa na wanachama wa chama chake.

Uamuzi wa kumtimua McCarthy umetolewa kwa pendekezo la Matt Gaetz, mmoja kati ya wawakilishi wa Republican wa jimbo la Florida na mshirika mwaminifu wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ambaye anaongoza sehemu ya wahafidhina wenye misimamo mikali katika Chama cha Republican.

Gaetz alimshutumu Spika McCarthy kwa kufanya makubaliano ya siri na Ikulu ya White House kuendelea kufadhili Ukraine, jambo ambalo Bw McCarthy amelikanusha.

Kura hiyo inajiri siku chache tu baada ya kutokea mgawanyiko ndani wa chama cha Republican ambao uliifanya serikali ya Marekani ikaribie kufungwa juu ya mjadala wa muswada wa kufadhili bajeti ya serikali ya nchi hiyo.Mpango wa kumuuzulu McCarthy uliotekelezwa na wanachama wenzake wenye msimamo mkali ulikuja baada ya kushirikiana na Wademocrat kuzuia kufungwa kwa utawala wa Biden. Warepublican na wafuasi wa Trump hawakufurahishwa na utendaji wa McCarthy kutokana na makubaliano yake na utawala wa Biden kuongeza kiwango cha deni na kupitisha bajeti ya muda mfupi.

342/