Main Title

source : Parstoday
Jumatano

4 Oktoba 2023

17:37:39
1397922

Russia yaripoti ukuaji mkubwa wa biashara na Afrika

Mauzo ya biashara kati ya Russia na nchi za Afrika yameongezeka kwa asilimia 43.5 katika miezi minane ya kwanza ya 2023 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita, RBK ya kila siku ya biashara iliripoti jana Jumatatu, ikinukuu Wizara ya Uchumi ya Russia.

Kwa upande wa fedha, kiasi cha biashara kilifikia dola bilioni 15.5, huku Misri, Algeria, Morocco, Tunisia na Libya zikitajwa kati ya washirika wakuu wa biashara wa Russia.

Waziri wa Uchumi wa Russia, Maksim Reshetnikov, amesema Afrika ina msingi mkubwa wa rasilimali, lakini hakuna teknolojia ya uzalishaji, na kuongeza kuwa teknolojia za Russia za kuchimba madini ni muhimu kwa Afrika.

Aidha amesema, Russia inaweza kuisaidia Afrika katika miradi ya ustawi wa miji kuipatia uzoefu katika ujenzi wa nyumba, barabara na reli, bandari, mabomba ya mafuta na gesi.

Mapema mwaka huu, Reshetnikov alitabiri kuwa biashara ya Russia na Afrika ingeongezeka maradufu ifikapo 2030.Mnamo 2022, Rais wa Russia, Vladimir Putin alisema mauzo ya biashara kati ya Russia na Afrika yalifikia dola bilioni 18. Wakati huo huo, Baraza la Shirikisho liliripoti kuwa mauzo ya nje ya Russia kwa mataifa ya Afrika yalifikia dola bilioni 14.8. Benki ya Russia hapo awali iliripoti kwamba 12.7% ya mauzo ya nje ya Russia kwa Afrika yalifanywa kwa kutumia sarafu ya rubles mnamo Julai 2023, wakati karibu 79% ya malipo yalifanywa kwa "sarafu zingine" ambazo zilijumuisha Yuan ya China, ikilinganishwa na 39% iliyorekodiwa katika Juni 2023.

342/