Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

6 Oktoba 2023

15:47:38
1398390

Wagonjwa 300 wafungua mashtaka kwa kudhalilishwa kingono na madaktari British Columbia Marekani

Wagonjwa 300 wanawake wamekishtaki Chuo Kikuu cha Columbia, kilichoko katika jimbo la British Columbia nchini Marekani, kwa kufanyiwa udhalilishaji wa kingono na madaktari wa chuo hicho.

Ubakaji na udhalilishaji wa kingono dhidi ya wanawake na watoto ni jambo lililozoeleka na la muda mrefu katika jamii ya Marekani, na linashuhudiwa katika sehemu nyingi za nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na vituo vya kijeshi, vya elimu, matibabu, na sehemu za kuhifadhi wahamiaji na watoto.

Kila baada ya muda, hutolewa takwimu za kufichuliwa kesi mbalimbali za ubakaji, ambazo kwa mtazamo wa wataalamu ni sawa na ncha ya mlima wa barafu unaoelea, kwa sababu waathiriwa wengi hukataa kutangaza na kufichua kesi hizo kwa sababu mbalimbali.

Katika mlolongo wa mashtaka hayo, madaktari na vituo kadhaa tanzu vya tiba vya Chuo Kikuu cha Columbia zimeshutumiwa kwa kuhusika na udhalilishaji wa kingono.

Kwa mujibu wa Newsweek, mmoja wa madaktari walioshtakiwa ni Robert Haden, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela mwezi Julai mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya makosa manne ya kuwabaka wagonjwa.

Jaji Berman, aliyeendesha kesi hiyo, alisema: vitendo vya Haden vimevuka mpaka wa tabia isiyo ya kawaida na ni mfano wa wazi wa miamala miovu ya kingono.

Berman aliongeza kuwa, wagonjwa wasiopungua 245 waliowahi kutibiwa na Haden wamedai kwamba aliwadhalilisha kingono.

Taasisi ambazo Haden aliwahi kufanya kazi, ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Columbia Irving Medical Center (CUIMC) na Hospitali ya New York-Presbyterian, tayari zimekubali kuchunguza kesi za madai za wagonjwa zaidi ya 200 waliotibiwa na daktari huyo.

Msemaji wa jimbo la British Columbia amesema wamesikitishwa na tabia na matendo ya daktari huyo.../

342/