Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

6 Oktoba 2023

15:50:19
1398395

Maseneta 20 wa Marekani wataka kukabiliwa utawala wa Kizayuni

Katika barua kwa Rais Joe Biden wa Marekani, wajumbe 20 wa chama cha Democratic katika Baraza la Seneti la Marekani wamemtaka aunge mkono suala la suluhu kati ya Wapalestina na utawala haramu wa Israel na kudhaminiwa usalama wa pande mbili.

Tor Winsland, mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Magharibi mwa Asia hivi karibuni alisisitiza juu ya ulazima wa kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa utawala wa Kizayuni na kusema katika kikao cha kila mwezi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili kuchunguza hali ya Asia Magharibi, kuwa kutokuwepo mpango wa amani kwa ajili ya kukomesha siasa za mabavu za Israel, kumepelekea kuendelea kwa hali mbaya katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Wajumbe wa Baraza la Seneti la Marekani pia wametilia mkazo ulazima wa kuzingatia kutotwaliwa sehemu yoyote ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kusimamisha mchakato wa sasa wa makazi, kuharibu vitongoji visivyoidhinishwa na visivyo vya kisheria katika Ukingo wa Magharibi na kusimamishwa utekeji wa baadhi ya maeneo ya Wapalestina.Maseneta hao wa Marekani pia wameutaka utawala wa Kizayuni kuiruhusu Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuendeleza mipango ya ujenzi inapobidi ili kukabiliana na tatizo la makazi linalosababishwa na ongezeko la watu. Miongoni mwa waliotia saini barua hiyo ni watu kama vile Chris Murphy, mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Asia Magharibi ya Congress, Dick Derbin, mwenyekiti wa Kamati ya Mahakama, kama mmoja wa viongozi wakuu wa Chama cha Dempcrats, Tim Kaine, aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais katika chama cha Democrats, Bernie Sanders, Elizabeth Varin na Maseneta wa Kiyahudi Bryan Schatz na John Asoff. Kwa mujibu wa azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ujenzi wa vitongozi vya wazayuni ni kinyume cha sheria. Kwa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuharibu nyumba za Wapalestina, utawala wa Kizayuni unajaribu kubadilisha muundo wa kijiografia wa maeneo ya Palestina ili kuimarisha utawala wake katika maeneo hayo.


/342