Ayatullah Riza Ramizani, Katibu Mkuu wa Baraza la Dunia la Ahlul-Bayt (AS) alihudhuria hafla hii kama mgeni mkuu na alikaribishwa kwa moyo mkunjufu. Katika kikao hicho chini ya uongozi wa Ayatullah Riza Ramizani, kituo cha Az-Zahra kilifunguliwa rasmi na kituo hicho kinaangazia shughuli za kidini za wanawake zinazohusiana na masuala ya kijamii na kiuchumi. Kisha katibu mkuu wa baraza la Ahlul-Bait (AS) akazuru kaburi la shahidi Abdulkadir ambaye aliuawa shahidi mikononi mwa Mawahabi, na akamuomba Mwenyezi Mungu ambariki marehemu.
342/