Main Title

source : Parstoday
Jumatano

11 Oktoba 2023

19:47:25
1400100

Zakzaky akiwa Tehran: Mapinduzi ya Kiislamu yataleta mabadiliko duniani

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) amesema anatumai Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yataleta mabadiliko na mageuzi katika kona zote za dunia.

Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema hayo leo Jumatano mara tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Imam Khomeini hapa Tehran akiwa ameandamana na mkewe, Malama Zeenah Ibrahim.

Ameeleza kuwa, "Sote tupo katika mtihani mkubwa, na inatarajiwa kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yataleta mabadiliko kote duniani ikiwemo Marekani na Ulaya, ili kuandaa mazingira ya kurejea Imam wa mwisho wa Mashia, Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake)."

Sheikh Zakzaky amesisitiza kuwa, fikra za Imam Khomeini ziko hai siku zote, kwa sababu Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anafuata nyayo zake.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema Iran inasonga mbele kwa kutegemea maarifa ya wataalamu na wasomi wa ndani na kutokana na kukata utegemezi kwa nchi za kigeni, na vijana wa Iran ni wavumbuzi katika nyanja mbalimbali za kisayansi.Sheikh Ibrahim Zakzaky amepokewa kwa moyo mkunjufu na umati mkubwa wa wananchi wa Iran, wafuasi wake pamoja na wanachuo. Waliompokea walikuwa wamebeba picha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). "Nina furaha mno kwa kujitokeza umati huu mkubwa hii leo kunipokea na kuunga mkono mapambano. Sina cha kusema, ila kukushukuruni sana," amesema Sheikh Zakzaky. Kiongozi huyo wa kidini wa Nigeria amewasili nchini Iran, ikiwa ni safari yake ya pili nje ya nchi, baada ya mamlaka za Abuja kumfutia kifungo cha nyumbani.

342/