Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

20 Oktoba 2023

19:54:18
1403172

Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Shambulio la Muqawama lililofanywa wakati mwafaka ni halali na linakubalika kimataifa

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesisitiza kuwa, shambulio liliofanywa wakati mwafaka la Muqawama ni halali na linakubalika katika uga wa kimataifa na dhamiri za umma; na halina pingamizi yoyote.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Kazem Sediqi amesema katika hotuba za Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran kwamba waziri mkuu mhalifu na mtenda jinai asiye na akili wa utawala wa Kizayuni hubomoa nyumba za watu kila mara, kwa hivyo kujihami kulikofanywa ni jambo la kimaumbile. Kwa mujibu wa ISNA, Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameongeza kuwa: Kwa muda wa miaka 70, nyumba za watu wa Gaza zimebomolewa, na wao wenyewe wameachwa bila makazi, wameuliwa na kuwekewa mzingiro. Hujjatul-Islam wal-Muslimin Seddiqi amebainisha kuwa: Wazayuni wana kila aina ya vifaa kama vile ukuta wa kizuizi, ambao wametumia mamilioni ya dola kuujenga na ambao hauna tofauti na ukuta wa Khaybar. Wameweka pia minara ya uangalizi, vitengo vya upelelezi, ndege zisizo na rubani za doria, wanapatiwa misaada ya kiintelijensia na kijasusi na Marekani na nchi kadhaa za Magharibi na wanapeleleza pia laini za simu za Wapalestina.Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameendelea kufafanua kwamba: Wazayuni hawakudhani kama maelfu ya wapiganaji wangeweza kuvivuka vizuizi hivyo kama umeme na kuziteketeza kambi za kijeshi na kuwaangamiza askari wa utawala unaoikalia Quds kwa mabavu na kurejea Gaza wakiwa na mateka chungu nzima.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Kazem Sediqi ameongeza kuwa: katika operesheni hiyo, ilivunjwa ile ngano na dhana kwamba kambi ya batili haiwezi kushindwa, lakini mkabala wake, badala ya kuwalenga wanamapambano wa Palestina, adui amebomoa nyumba za watu na kuwaua watoto, mama na baba zao; na kilichotokea Gaza ni maafa makubwa na mauaji ya kimbari. Katika sehemu nyingine ya khutba zake, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameendelea kusema: katika kilele cha uovu na ukatili huo, adui ameshambulia kwa makombora hospitali na skuli, ambazo ni kimbilio na maeneo ya kutoa hifadhi kwa raia, lakini mashambulio hayo yameamsha hisia safi za utu ulimwenguni kiasi kwamba sasa hivi utawala wa Marekani, Wamagharibi na utawala wa Kizayuni ndizo nyuso na tawala zinazochukiza zaidi mbele ya walimwengu.../


342/