Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

20 Oktoba 2023

19:54:49
1403173

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria: Kimbunga cha Al-Aqsa ni mwanzo wa kushindwa utawala wa Kizayuni

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (NIM) amesisitiza kuwa: operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni mwanzo wa kushindwa na kurudi nyuma jeshi lenye nguvu bandia la utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa IRNA, Sheikh Ibrahim Zakzaky, amesema katika hotuba aliyotoa kabla ya Khutba ya Sala ya Ijumaa mjini Mashhad ya kwamba: Wananchi wa Palestina wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa na kuuliwa kwa umati na Wazayuni kwa kipindi cha miaka 70 sasa; na katika miaka ya karibuni Waislamu duniani wamekuwa wakishuhudia jinsi Wazayuni wanavyouvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa. Sheikh Zakzaky ameashiria jinai za Israel na mashambulio iliyofanya dhidi ya Hospitali ya Al-Ma'madani, na akaongezea kwa kusema: kilichotokea katika operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni jibu kwa jinai zilizofanywa na Israel katika kipindi cha miaka 70 iliyopita.Kwa mujibu wa Zakzaky, operesheni hii ni moja ya sababu zilizoonyesha jinsi vituo vya kiintelijensia na kijasusi vya Israel vilivyo dhaifu na visivyo na uimara, kiasi kwamba vilishindwa kupata taarifa yoyote kuhusu kuanza kwa Kimbunga cha Al-Aqsa na havikuweza kukizuia.

 Aidha, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema: katika kukabiliana na operesheni ya mujahidina wa Palestina, utawala wa Kizayuni unawalenga watoto, wanawake na watu wasio na ulinzi kwa mashambulizi ya angani, jambo linaloonyesha udhaifu na woga ulionao utawala huo.Katika kukabiliana na jinai za Wazayuni, vikosi vya Muqawama wa Palestina siku ya Jumamosi ya tarehe 7 Oktoba, vilianzisha operesheni kubwa na ya kipekee iitwayo Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Ukanda wa Gaza (kusini mwa Palestina) dhidi ya ngome za utawala khabithi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.Kutokana na kushindwa vibaya sana kwa kuangamizwa Wazayuni zaidi ya elfu moja na kutekwa kwa muda baadhi ya vitongoji vya walowezi na vituo vya kijeshi, viongozi wa utawala huo ghasibu wameamuru kufanywa mashambulio ya kinyama ya mtawalia yanayowalenga Wapalestina wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza na kutenda jinai chungu nzima za kivita katika eneo hilo lililowekewa mzingiro.../


342/