Main Title

source : Parstoday
Jumapili

22 Oktoba 2023

15:54:52
1403974

Gaza: Israel imevunja kabisa misikiti 31 na kuharibu vibaya makanisa 3

Ofisi ya Vyombo ya Habari vya Serikali ya Ukanda wa Gaza imetangaza leo Jumapili kwamba idadi ya misikiti iliyovunjwa kabisa katika mashambulizi ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza imeongezeka na kufikia misikiti 31, na uharibifu mkubwa umerekodiwa katika makanisa 3.

Kwa upande wake, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Palestina imetangaza katika taarifa yake kwamba jeshi la Israel limeharibu kabisa misikiti 5 katika Ukanda wa Gaza, na hivyo kuifanya idadi ya misikiti iliyoharibiwa kufikia 31 tangu kuanza operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa tarehe 7 mwezi huu. 

Jumamosi iliyopita wizara hiyo ilikuwa imetangaza kwamba, mashambulio ya Israel yalikuwa yamevunja kabisa misikiti 26 Ukanda wa Gaza na kuharibu makumi ya misikiti.Vilevile, wafanyakazi 10 wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini wameuawa shahidi katika mashambulizi hayo ya Israel na wengine wengi wamejeruhiwa, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Makanisa pia hayakusalimika na mashambulizi ya Israel, kwani Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Serikali huko Gaza imeripoti uharibifu mkubwa kwenye makanisa 3.

Raia wengi wa Palestina waliuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa katika hujuma wa utawala haramu wa Israel Alhamisi iliyopita ambayo ililenga Kanisa la Kiorthodoksi, linalotambuliwa kuwa kanisa la tatu kongwe zaidi duniani, katikati mwa Jiji la Gaza.

Kanisa la Kiorthodoksi la Mtakatifu Porphyrios ndilo kanisa kongwe zaidi katika Ukanda wa Gaza ambalo bado liko wazi. Kanisa hilo liko karibu na msikiti katika Mji wa Kale wa Gaza, na lilijengwa juu ya kaburi la Mtakatifu Porphyrios.Kanisa hilo liko karibu na Hospitali ya Kibaptisti, ambayo Jumanne iliyopita ilikuwa uwanja wa mauaji ya kikatili ya mamia ya wagonjwa, watoto, wauguzi na madaktari wa Kipalestina katika shambulizi la kombora la jeshi la Israel. Jamii ya kimataifa imelaani vikali shambulizi na mauaji hayo yaliyofanywa na Israel na kuyataja kuwa ni uhalifu wa kivita. Nchi za Magharibi zinajaribu kupotosha ukweli kwa kutoa madai yasiyo na mashiko kuhusu shambulizi hilo la kikati na kuuondoa hatiani utawala wa kibaguzi wa Israel.  

342/