Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

26 Oktoba 2023

16:04:15
1405367

Idadi ya Wapalestina waliouawa Gaza yapindukia 7000

Ofisi ya Habari ya serikali huko Gaza Palestina imetangaza kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu utawala haramu wa Israel ulipoanza kufanya mashambulio ya anga katika Ukanda wa Gaza imepindukia 7000 huku makumi ya maelfu ya wengine wakiwa wamejeruhiwa au kutoweka.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, wengi wa mashahidi hao ni wanawake na watoto huku hali ya kibidamu katika Ukanda wa Gaza ikielezwa kuwa inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

Takwimu hizo zinatolewa katika hali ambayo, duru mbalimbali za habari zimetangaza kuwa, mashambulio ya anga ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza yanngali yanaendelea.

Tangu kuanza kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa siku 16 zilizopita sawa na Oktoba 7, kushambuliwa maeneo ya makazi na umma kwa upande mmoja na kukatwa maji, umeme na uhaba mkubwa wa chakula na dawa kwa upande mwingine, kumewafanya wakazi wa Ukanda wa Gaza kukabiliwa na hali ngumu sana na kupelekea taasisi za haki za binadamu kutangaza hali ya kibinadamu katika eneo hilo kuwa mbaya na ya kutisha. 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, waungaji mkono wa wananchi wa Palestina katika maeneo mbalimbali ulimwenguni wameendelea kujitokeza na kuandamana wakilaani jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza.Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limeonya kuhusu tishio linalokabili maisha ya watu wa Gaza. Wakati huo huo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu imeonya kwamba, unga wa ngano katika Ukanda wa Gaza utaisha katika muda wa chini ya wiki moja. Ashraf al-Qadara, msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, amesema mapema leo kwamba hawawezi tena kutoa huduma yoyote katika hospitali za Ukanda wa Gaza, na kwamba mfumo wa afya wa eneo hilo linalozingirwa na Israel unaporomoka kikamilifu.

342/