Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

30 Oktoba 2023

16:55:33
1406793

Amir Abdollahian azungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Qatar; wajadili matukio ya Gaza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri Mkuu wa Qatar wamezungumza kwa simu na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya Gaza.

Katika mazungumzo hayo, Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejadili na kubadilishana mawazo na Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Sheikh Muhammad bin Abdulrahman Al Thani kuhusu matukio ya karibuni ya Palestina na Ukanda wa Gaza. 

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar pia wamezungumzia udharura wa kusitishwa haraka iwezekanavyo mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kutumwa misaada endelevu na mikubwa ya kibinadamu kwa ajili ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. 

342/