Main Title

source : Parstoday
Jumanne

31 Oktoba 2023

15:30:40
1407181

Watoto waliouawa Gaza katika wiki 3 ni wengi kuliko migogoro yote ya kimataifa kila mwaka tangu 2019

Takwimu zilizoripotiwa na shirika la misaada la Save the Children zinaonyesha idadi ya watoto waliouawa katika Ukanda wa Gaza kutokana na uvamizi unaoendelea wa Israel imepita takwimu za kila mwaka zinazohusiana na migogoro ya kimataifa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Mashambulizi ya kikatili ya kijeshi ya Israel dhidi ya Gaza, yaliyoanza tarehe 7 Oktoba kujibu operesheni ya kundi la muqawama la Palestina Hamas, yamesababisha vifo vya watoto zaidi ya 3,000, zaidi ya idadi ya kila mwaka ya watoto waliouawa katika mapigano ya kivita duniani katika kila moja ya miaka minne iliyopita, limesema shirika hilo la kimataifa.

Shirika hilo la misaada lenye makao yake makuu nchini Uingereza lilitaja takwimu za Umoja wa Mataifa zinazoonyesha idadi ya watoto waliouawa katika migogoro katika nchi 24 mwaka jana ilikuwa 2,985, kutoka 2,515 waliouawa mwaka 2021 na 2,674 mwaka 2020.

Jason Lee, mkurugenzi wa nchi ya Save the Children katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, alisema idadi ya vifo miongoni mwa watoto huko Gaza inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na uvamizi unaoendelea wa utawala katili wa Israel.Hiyo ina maana kwamba idadi hiyo inaweza kufikia rekodi ya kila mwaka ya 4,019 iliyoripotiwa mwaka 2019 kulingana na ripoti ya mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya silaha.

Takwimu zilizotolewa na mamlaka ya afya huko Gaza siku ya Jumatatu zilionyesha baadhi ya watoto 3,457 wamekufa katika zaidi ya wiki tatu za mashambulizi ya Israel na makombora katika eneo hilo.

Jumla ya waliouawa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza ilifikia 8,306 siku ya Jumatatu, ambapo 2,136 walikuwa wanawake.


342/