Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

2 Novemba 2023

15:47:28
1407839

Meja Jenerali Salami: Sasa hivi dunia imeungana pamoja zaidi dhidi ya Marekani kupita wakati wowote ule

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema, sasa hivi miale ya Jihadi imewashwa na akaongeza kuwa: ulimwengu umeungana pamoja zaidi dhidi ya Marekani leo hii kupita wakati mwingine wowote ule; na dhati halisii ya umwagaji damu ya sera za nchi hiyo inadhihirika waziwazi ulimwenguni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Meja Jenerali Hossein Salami ameyasema hayo leo katika kongamano la maimamu wa misikiti na makamanda wa vituo vya Jeshi la kujitolea la Basij mjini Tehran na akaongeza kuwa: Marekani, Uingereza na Uzayuni ni pande tatu za uhalisia mchungu na sehemu zisizoweza kutenganika za njama na ukhabithi ulio dhahiri kabisa.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Wazayuni waliighusubu na kuipora Palestina miaka 75 iliyopita kwa jinai na ugaidi, na leo hii pia wanadhamiria kufanya hivyo ili vijana katika Ulimwengu wa Kiislamu waingiwe na upofu wa kisiasa, lakini wakati bendera ya utawala mkuu wa Kiislamu (Wilayat) inapopeperushwa, hapabakii njia yoyote kwa waistikbari na mabeberu ya kuuhadaa Umma wa Kiislamu.

Kamanda Salami ameongeza kuwa: Wazayuni walianzisha vita kadha wa kadha, lakini wakati huu wa uhai wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, maadui wamehakikisha wanaelekeza kila vita katika ardhi za Kiislamu, na tangu miaka 45 iliyopita, Uistikbari umezitumbukiza kwenye vita ardhi za Kiislamu ili isiweze kujengeka na kupatikana nguvu kwa jina la Uislamu.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amebeainisha kuwa: leo wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza wamejaza ndani ya nyoyo za Waislamu uwezo wa kulipiza kisasi wa makumi ya miaka, na hali ya utata mkubwa zaidi inayoitatiza Marekani ni kushindwa kutoa tafsiri ya ushindi katika Ukanda wa Gaza.../

342/