Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

4 Novemba 2023

15:03:39
1408340

Spika wa Bunge la Iran: Oparesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa imebadilisha mlingano wa kimataifa

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu la Iran amesema: Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ilibadilisha m mpangilio mlingano wa mfumo wa kimataifa.

Mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, wanajeshi wa makundi  ya wapigania ukombozi au wanamuqawama wa Palestina walianzisha operesheni ya kushtukiza iitwayo "Kimbunga cha Al-Aqsa" kutoka Gaza (kusini mwa Palestina) dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni wa Israel ili kujibu jinai za mara kwa mara za utawala huo dhidi ya Wapalestina. Katika kulipiza kisasi pigo hilo la kihistoria, utawala ghasibu wa Israel ulishadidisha mzingiro katika Ukanda wa Gaza na tokea siku hiyo umekuwa ukidondosha mabomu dhidi ya raia wa Gaza.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina ametangaza kuwa, idadi ya mashahidi huko Gaza imefikia zaidi ya elfu 9,200 na idadi ya waliojeruhiwa imefikia zaidi ya elfu 23.

Kuhusiana na hili, Mohammad Baqir Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran katika hotuba kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa ameeleza kuwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ilibadilisha malingano wa mfumo wa  dunia na kuongeza kuwa: "Vyovyote vile wafanyavyo, wakuu wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel hawawezi kuirejesha dunia katika hali ya awali ya kabla ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa."

Akigusia uungaji mkono wa watetezi wa uhuru duniani kwa watu wa Gaza na Palestina, Spika Bunge la Iran amesema: "Mwisho wa njia ya mchakato kuanzisha uhusiano na Israe ni kushindwa na kufilisika na na mwisho wa njia ya muqawama na mapambano  ni ushindi, fahari na heshima.

342/