Main Title

source : Parstoday
Jumapili

5 Novemba 2023

17:53:20
1408815

Putin: Ni nyoyo za mawe tu ndizo zisizohisi chochote zinapoona picha za watoto wa Gaza

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema katika kuzungumzia jinai za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwamba: "unapowatazama watoto wanaoteseka na walioroa damu wa Gaza, ngumi zako zinakunjamana, na macho yako yanabubujikwa na machozi".

Kwa mujibu wa shirika la habari la Anatolia, Putin amesema ni wale tu wenye "moyo wa jiwe" ndio wanaoweza kuyatazama bila kuhisi chochote matukio ya Ukanda wa Gaza, mahali ambapo hadi sasa karibu raia 10,000 wameuawa na Wapalestina wapatao 35,000 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israel.

Katika kikao alichofanya siku ya Ijumaa na maulamaa wa Kiislamu nchini Russia, Rais huyo wa Shirikisho la Russia alikosoa jinai za utawala wa Kizayuni na mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya raia wa Gaza.Mashambulio ya kinyama dhidi ya Gaza na mauaji ya kikatili ya wanawake na watoto wa Kipalestina katika eneo hilo yangali yanaendelea huku nchi za Magharibi zinazouunga mkono utawala wa Kizayuni zikiwa zimepigia hadi sasa kura ya veto kila azimio la usitishaji vita lililowasilshwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na badala ya kufanya juhudi za kusimamisha mauaji na mashambulizi dhidi ya Wapalestina wanafikiria kupitisha maazimio ya kuuunga mkono zaidi tawala wa Kizayuni. Mwakilishi wa Russia katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alipendekeza azimio la kulaani jinai za utawala wa Kizayuni lakini lilipigiwa kura ya turufu na Marekani.../

342/