Main Title

source : Parstoday
Jumapili

5 Novemba 2023

17:54:02
1408816

Mbunge wa Marekani asema: Biden anasaidia mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina

Mbunge mmoja wa Baraza la Congress ya Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic amesema kuwa, rais wa nchi hiyo, Joe Biden anasaidia moja kwa moja mauaji ya umati na maangamizi ya kizazi dhidi ya Wapalestina na kwamba Wamarekani hawatolisahau hilo katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2024.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo leo na kumnukuu Mbunge Rashida Tlaib wa chama cha Biden cha Democratic akimtaka rais huyo wa Marekani aulazimishe utawala wa Kizayuni ukomeshe mauaji ya kizazi huko Ghaza. Bi Rashiida Tlaib ndiye mbunge pekee mwenye asili ya Palestina katika bunge la Marekani. 

Amemkhutubu Biden akimwambia, Wamarekani hawakuungi mkono katika msimamo na hatua zako hizi dhidi ya Wapalestina. Wamarekani hawatolisahau jambo hilo katika uchaguzi wa rais wa 2024.

Amemwambia: "Biden unga mkono juhudi za kukomesha mapigano Ghaza vinginevyo usitutarajie kukuunga mkono katika uchaguzi wa 2024."

Rais wa Marekani, Joe Biden pamoja na uzee na kigugumizi na uzito wake wa kuzungumza lakini mara kwa mara amekuwa akisikika akisema kuwa, serikali yake itaendelea kuisaidia Israel katika vita vyake dhidi ya HAMAS.Uchunguzi mbalimbali wa maoni ukiwemo wa taasisi za Economist na YouGov unaonesha kuwa, asilimia 22 tu ya wanachama wa chama cha Democratic cha Biden ndio wanaounga mkono kuendelea kupewa silaha utawala wa Kizayuni. Amma kwa upande wa chama cha Republican, asilimia 48 ya wabunge wake wanaunga mkono jambo hilo. Asilimia 45 ya Wademocratic wanataka misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina iongezwe huku asilimia 8 tu ya Warepublican wakiunga mkono misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina. Hii ni katika hali ambayo, afisa mwingine mmoja wa ngazi za juu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ametangaza kupinga waziwazi siasa za Biden za kuunga mkono utawala katili wa Israel na kumlaumu moja kwa moja kwamba anahusika kikamilifu na mauaji ya halaiki huko Ghaza.

342/