Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

6 Novemba 2023

16:43:04
1409206

Amir Abdollahian: Jamii ya kimataifa inapasa kuhamasishwa ili kuzuia kutokea maafa Gaza

Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza katika mawasiliano yake ya pili rasmi na Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tangu kuanza vita huko Gaza kwamba: Jamii ya kimataifa inapasa kuhamasishwa ili kuzuia kutokea maafa na Nakba nyingine katika ardhi za Palestina.

Katika mazungumzo hayo, Hossein Amir Abdollahian ametaja kuharibiwa na kubomolewa kwa makusudi miundombinu ya mji na idara, hospitali, vituo vya elimu na shule kuwa ni jambo la kutisha kwa ulimwengu kuwahi kulishuhudiwa katika karne ya karibuni na kusema: Mshambulizi ya nchi kavu ya utawala wa Kizayuni na kutochukua hatua jamii ya kimataifa ili kusitisha hujuma hizo kutaanda uwanja wa kujiri maangamizi ya kizazi.   

Amir Abdollahian ametaja vitendo vya utawala wa Kizayuni katika mashambulizi yake ya kikatili ya hivi kkaribuni huko Ukanda wa Gaza kuwa ni jinai ya kivita na akasema, utawala huo hadi sasa umekiuka maazimio zaidi ya 30 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na akatilia maanani uzingatiaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa baadhi ya ukiukwaji wa wazi wa sheria na kanuni za kimataifa na haki za binadamu katika kipindi cha miaka 75 ya kukaliwa kwa mabavu na Israel ardhi za Palestina.   

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amemtaka Antonio Guterres pamoja na kulaani ukikwaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala wa Kizayuni achukue hatua za lazima ili kuhitimisha haraka na bila ya masharti mashambulizi ya utawala wa Kizayuni, kuondolewa mzingiro wa Gaza na kuwezesha upatatikanaji huru wa misaada ya kibinadamu ya kimataifa kwa raia wa Kipalestina wa  Ukanda wa Gaza. 

Wizara ya Afya ya Gaza jana ilitangaza kuwa watu 9,770 wameuliwa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7 hadi sasa; ambapo kati ya mashahidi hao watoto ni 4,800, wanawake 2,550 na wazee 596. Wizara hiyo aidha imetangaza kuwa watu elfu 24 na 808 wamejeruhiwa hadi sasa katika mashambulizi ya kikatili ya utawala haramu wa Israel huko Gaza. 


342/