Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

9 Novemba 2023

17:26:54
1410095

Mkusanyiko wa wafanyakazi wa bunge la Marekani kwa ajili ya kusitisha mapigano Gaza

Wafanyakazi wa Bunge la Marekani, wamekusanyika mbele ya jengo hilo, wakidai kusitishwa mapigano huko Gaza.

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetangaza kuwa zaidi ya Wapalestina 10,700 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala ghasibu wa Kizayuni tangu kuanza vita katika ukanda huo kufuatia operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa tarehe 7 Oktoba.

Kwa mujibu wa ripoti ya Alkhamisi ya ISNA, kundi la wafanyakazi wa Kongresi ya Marekani pamoja na kutoa heshima zao kwa wahanga wa jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza, limetoa wito wa kusitishwa mapigano katika eneo hilo haraka iwezekanavyo.

Kundi hilo linalojiita Wafanyakazi wa Congress kwa ajili ya Kusitishwa Mapigano, "Congress Staff for a Ceasefire" , limewashutumu viongozi wa bunge hilo katika taarifa kwa kutozingatia takwa lao la kusitisha vita huko Ghaza.Taarifa hiyo inasema: 'Tunataka kusitishwa mapigano huko Ghaza, kusimamishwa haraka vita katika eneo na kuachiliwa mateka.' Wafanyakazi hao pia wameweka mashada ya maua mbele ya jengo la Bunge la Marekani na kukaa kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa wahanga wa mgogoro unaoendelea huko Ghaza. Kuhusiana na suala hilo, Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema leo kwamba: 'Kinachoendelea katika Ukanda wa Gaza ni mauaji ya halaiki na lazima yakomeshwe mara moja.'

342/