Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

13 Novemba 2023

19:32:58
1411244

Kan'ani: Jinai ya Wazayuni ya kushambulia hospitali ni matunda ya kimya cha jamii ya kimataifa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema huku akiwa ameshikilia picha za hospitali ya al Shifa ya Ghaza kwamba: "Baada ya walimwengu kunyamaza kimya wakati Wazayuni waliposhamblia hospitali ya Al-Ma'amadani, utawala wa Kizayuni ulizidi kupanda kiburi cha kushambulia hospitali nyinginezo za Ghaza ikiwemo ya al Shifa.

Shirika la Habari la Iran Press limemnukuu Nasser Kan'ani, akisema hayo na kuongeza kuwa: Utawala wa Kizayuni umeizingira kikamilifu Hospitali ya al Shifa huko Gaza na unaishambulia kwa risasi, licha ya kwamba kumejaa mabango kila upande yanayotahadharisha na kusisitizia wajibu wa kuchungwa utulivu kwenye eneo hilo la hospitali.

Ameongeza kuwa: "Ni jukumu la walimwengu kusimama dhidi ya utawala wa wa Kizayuni."

Lakini utawala huo pandikizi ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani na madola ya Magharibi unaendelea kufanya jinai kubwa kupindukia ambazo hakuna maneno yanayoweza kuakisi ukubwa wa jinai na ukatili huo wa Wazayuni.Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema: Tunatamani kuuona Umoja wa Mataifa unatekeleza ipasavyo majukumu yake na kuhakikisha jinai za Wazayuni zinakomeshwa huko Ghaza. Amma kuhusu misimamo ya serikali ya Marekani, Nasser Kanani amesema: "Marekani inataka kupotosha fikra za walimwengu kwa kuendelea kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Iran. Tumeeleza mara chungu nzima kwamba makundi ya muqawama katika eneo hayachukui amri kutoka Iran bali yanafanya mambo yao baada ya kupiga mahesabu na kuzingatia maslahi yao wenyewe." Amesisitiza kwa kusema: "Iran imekuwa ikionya mara kwa mara kuhusu hatari za kuenea vita kutokana na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni na imekuwa ikisema wazi kwamba jinai za Wazayuni na uungaji mkono huo wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni unaweza kusababisha kuenea vita na katika eneo hili." 

342/