Main Title

source : Parstoday
Jumanne

14 Novemba 2023

18:56:28
1411592

White House: Hatuna taarifa kuhusu mahali walipo mateka wa Kizayuni huko Gaza

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa White House amesema kuwa kuna haja ya kusitishwa vita kwa siku kadhaa ili kuwaachia huru mateka wa Kizayuni wanaoshikiliwa Ukanda wa Gaza.

Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa, Jack Sullivan Mshauri wa Usalama wa Taifa wa White House jana usiku alizungumza na waandishi wa habari na kusema: Marekani inaendelea kufanya juhudi ili kufanikisha kuachiwa huru Wazayuni waliotekwanyara na Hamas.  

Sullivan alifafanua kuhusu kutumia neno usitishaji vita wa kimkakati wa kibinadamu kwamba na hapa ninakuu:" Tunaendelea kuzungumza na Israel kuhusu umuhimu wa kufikia usitishaji vita wa kimbinu wa kibinadamu, mwisho wa kunukuu."  

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa White House ameeleza kuwa Marekani haina taarifa za wazi kuhusu mahali na hali waliyonayo mateka wa Kizayuni huko Gaza na kuongeza kuwa:" tunataka kushuhudia mapatano ya kibinadamu ya siku kadhaa katika fremu ya kuwaachia huru mateka." 

Afisa huyo wa Marekani amedai kuwa: Hospitali za Gaza lazima ziwe na uwezo wa kufanya kazi ili kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa. Ameendelea kudai kuwa:Tunaamini kuwa usitishaji vita  haupaswi kuwekewa ratiba kali, bali unapaswa kufikia malengo ya kuhakikisha misaada inafikishwa katika hali ya usalama.

Wakati huo huo, Ofisi ya Upashaji Habari ya Serikali huko Gaza imetangaza kuwa hadi sasa idadi ya watu waliouliwa shahidi Ukanda wa Gaza imefika 11,240; ambapo watoto ni 4,630 na wanawake ni 3,130.