Main Title

source : Parstoday
Jumanne

14 Novemba 2023

18:59:09
1411598

Khaled Qaddoumi: Joe Biden anasimamia vita vya Gaza

Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) nchini Iran amesema kuwa, Rais wa Marekani, Joe Biden ndiye anayesimamia vita na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

Khaled Qaddoumi amesema katika kikao cha tatu cha Jukwaa la Wanaodhulumiwa Duniani kinachoangazia zaidi vita vya Gaza na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kinachofanyika mjini Tehran, kwamba Rais Joe Biden na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken wanashiriki katika chumba cha vita cha utawala wa Kizayuni mjini Tel Aviv.

Mwakilishi wa Hamas nchini Iran amesema kuwa, vita vya sasa si kati ya Palestina na Israel, bali ni kati ya Uislamu na ubeberu, na kuongeza kuwa iwapo Gaza itashindwa, itakuwa zamu ya Beirut, Amman, Cairo na maeneo mengine.

Hapo awali duru za ndani za Palestina zilithibitisha kwamba wanajeshi wa Marekani wanashirikiana na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.

Himaya na ushirikiano wa Marekani na utawala wa kigaidi wa Israel unaoendelea kuua raia wa Palestina wasio na hatia hususan watoto wadogo, vimeendelea kulaaniwa kote duniani. Taasisi mbalimbali za kimataifa kama Amnesty International, UNICEF na timu ya wataalamu ya Umoja wa Mataifa zinasema mashambulizi hayo yanakiuka sheria za kimataifa bali ni uhalifu wa kivita. 

Zaidi ya Wapalestina elfu 11 na mia mbili wameuawa shahidi hadi sasa katika mashambulizi ya Israel huko Ukanda wa Gaza, zaidi ya elfu 8 miongoni mwao wakiwa watoto na wanawake.  

342/