Main Title

source : Parstoday
Jumatano

15 Novemba 2023

20:23:51
1411967

Mafuta ya Russia bado yanadhamini mahitaji ya jeshi la Marekani

Utafiti wa gazeti la Washington Post unaonyesha kuwa mafuta ya Russia yanaendelea kukidhi mahitaji ya jeshi la Marekani licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Moscow.

Kwa mujibu wa jarida la Focus la Ujerumani, utafiti wa gazeti la Washington Post unaonyesha kuwa licha ya vikwazo vya mafuta vya nchi za Magharibi dhidi ya Russia, lakini bidhaa za mafuta za nchi hiyo zinafika Marekani kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Ugiriki kinachokidhi mahitaji ya mafuta ya jeshi la Marekani.

Kulingana na ripoti hiyo, kiwango asili cha mafuta ya Russia hakijulikani kutokana na kutokuwepo nyaraka na kufanyika mabadiliko mengi katika umiliki wa bidhaa hiyo.

Ni vigumu sana kujua ukweli wa mambo kutokana na kuwa  kiwanda hicho cha kusafisha mafuta kimeacha rasmi kupokea mafuta kutoka Russia na kupata vyanzo vingine.

342/