Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

18 Novemba 2023

15:25:45
1412803

Ofisi ya Iran UN: Muundo wa sasa wa Baraza la Usalama hauakisi hali halisi ya jamii ya kimataifa

Afisa wa kitengo cha habari wa ofisi ya mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema: Muundo wa sasa wa Baraza la Usalama la umoja wa huo hauakisi hali halisi ya jamii ya kimataifa.

Ali Karimi Moghadam, aliyekuwa akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York unaojadili suala la kurekebisha muundo wa sasa wa Baraza la Usalama, ameashiria utochukua hatua kwa taasisi hiyo mbele ya jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa Palestine na kusema kuwa: Kushindwa kwa kiasi kikubwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua na kuuwajibisha utawala wa Israel kwa kutenda jinai za kivita dhidi ya wananchi wa Palestina ni ishara tosha ya haja ya kufanya mabadiliko ya kimsingi katika taasisi hii ya kimataifa.

Karimi Moghadam amesema: "Hakuna kinachoweza kuhalalisha jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika hali ambayo, kwa masikitiko makubwa, Baraza la Usalama halijachukuia hatua yoyote ya kushughulikia jinai hizo."

Mwanadiplomasia huyo wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema: Baraza la Usalama ambalo lilipaswa kusaidia juhudi za kudumisha amani, sasa limeuwezesha utawala wa Israel kuendelea kutenda uhalifu na jinai zake za kivita huko Gaza, na hakuna adhabu yoyote inayoukabili utawala huo ghasibu.Israel inaendeleza mauaji ya wanawake na watoto wa Kipalestina katikak Ukanda wa Gaza huku nchi za Magharibi zinazouunga mkono utawala huo zikipiga kura ya veto ya kuzuia azimio lolote la usitishaji vita katika Baraza la Usalama. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, zaidi ya Wapalestina elfu 12 wameuawa shahidi na zaidi ya watu elfu 29 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, kutokana na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.

342/